
Barack Obama wakati wa sherehe ya kuapishwa kuwa Rais Donald Trump. Picha; Hisani

Picha; Hisani
Na Zillah Zillah,
Aliyekuwa rais wa 44 wa Marekani Barack Obama amehudhuria sherehe ya kuapishwa kuwa Rais Donald Trump pekee yake, huku Michelle Obama akikosa kuhudhuria kwa mara ya pili.
Ofisi ya Obama ilithibitisha mapema kuwa Michelle hatashiriki, bila kutoa sababu rasmi.
Chanzo kilisema Michelle alikataa kuhudhuria kwa sababu hana unafiki na mara zote amekuwa makini kuhusu mahali anapojitokeza.
Wakati huo, Barack Obama alionekana kuwa na mazungumzo ya kirafiki na Trump kwenye mazishi ya Rais Jimmy Carter, hali iliyozua maoni tofauti.
Tetesi za ndoa yao kuzorota zimeendelea, lakini Barack Obama alikanusha kwa kumpa Michelle ujumbe wa mapenzi kwenye siku yake ya kuzaliwa, akimtaja kama “mpenzi wa maisha yake.”
Wanandoa hawa walioana mwaka 1992 na wana mabinti wawili, Malia na Sasha.